Msikiti Mkuu wa mji wa Taipei, ni moja ya majengo muhimu sana katika makao makuu hayo ya Taiwan. Huo ndio Msikiti mkubwa zaidi na maarufu zaidi huko Taiwan. Una ukubwa wa wa mita mraba 2747.

Msikiti huo uko kwenye wilaya ya Da’an katika jiji la Taipei. Naam, ni moja ya majengo muhimu sana ya Kiislamu huko Taiwan.

Tarehe 29 Juni 1999, Msikiti huo ulisajiliwa na mamlaka ya Taipei kuwa moja ya majengo muhimu ya kihistoriana kiutalii.

Msikiti huo ulijengwa mwaka 1947 na ulikarabatiwa mwaka 1960 na kuwa na muundo na sura yake ya hivi sasa.

Ukumbi wa Msikiti huo ulijengwa kulingana na utamaduni wa Kiislamu ambapo wakuu wa Taiwan walijenga Msikiti huo kuonesha wana uhusiano mzuri na nchi za Kiislamu. Msikiti huo umesaidia kuimarika uhusiano wa kidiplomasia baina ya Taiwan na nchi za Kiislamu.

Baada ya kujengwa Msikiti huo, kulipatikana msukumo wa kujengwa Misikiti mingine kama ule wa Kaohsiung, Msikiti wa kiutamadui wa Taipei na Msikiti wa Taichung.

Msikiti huo una uwezo wa kupokea Waislamu 1,000 kwa wakati mmoja. Mazulia na vigae vya madirisha yake ni kutoka Uajemi yaani Iran.

Awali Waislamu walikuwa wakisali tu katika ghorofa ya kwanza ya Msikiti Mkuu wa Taipei. Hata hivyo idadi ya Waislamu ilipoongezeka, sasa ghorofa ya pili ya Msikiti huo ni maalumu kwa Waislamu wanawake na ghorofa ya chini inajaa wanaume. Huduma nyingine zilizopo Msikitini hapo ni ukumbi wa wageni, ofisi ya uongozi wa Msikiti, Maktaba na sehemu nyingine muhimu na za lazima kwa kila Msikiti.

Hapa tumeweka kipande cha video kuhusu Msikiti huo

Na hapa chini ni baadhi ya picha ya Msikiti huo

(Visited 134 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!