Miongoni mwa sifa za kipekee za misahafu hiyo ni kwamba kila ukurasa unamalizikia na mwisho wa aya. Yaani hakuna aya yoyote katika khati za Taha inayokatika kipande na kumalizikia ukurasa mwingine. Uwazi na usomekaji wa kiurahisi wa khati za Uthman Taha ni sifa nyingine inayoifanya misahafu iliyoandikwa kwa khati hizo kupendwa na kuenea dunia nzima.

Uthman Taha ni nani?

Tumetangulia kusema kwamba jina lake kamili ni Uthman ibn Abduh ibn Husayn ibn Taha al Kurdi. Alizaliwa mwaka 1934 katika kijiji kimoja cha mkoani Halab (Aleppo) nchini Syria na sasa hivi ana umri wa miaka 86.

Katika umri wake Uthman Taha ameshaandika Qur’ani nzima mara 12 kwa khati zake kwenye Kituo cha Mfalme Fahd cha Uchapishaji Qur’ani Tukufu katika mji mtakatifu wa Madina.

Uthman Taha

Masomo Yake

Uthman Taha alianza masomo yake huko huko Halab (Aleppo) Syria. Baba yake pia alikuwa bingwa wa khati za Kiarabu na alitumia sana khati za Ruq’ah. Uthman Taha alisoma fani ya khati pamoja na mabingwa wa khati kama vile Mohammed al Mawlawi, Mohammed al Khatib, Hussein al Turki na Ibrahim al Rifai. Baada ya kujifunza khati kutoka kwa baba yake, Uthman Taha alielekea Damascus, mji mkuu wa Syria kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu na huko alianza kujifunza aina nyingine za khati kama vile Thuluth na Naskh ambayo hivi sasa anahesabiwa kuwa ni bingwa wa khati hiyo. Alijifunza pia khati ya Farsi. Alipata cheti chake cha shahada ya uzamili (master degree) katika fani ya khati kutoka kwa mwandishi bingwa wa khati, Hamed al Amadi mwaka 1973.

Kuhamia Saudi Arabia

Mwaka 1988 Uthman Taha alianza kufanya kazi ya uandikaji wa Qur’ani Tukufu katika Muassasa wa Mfalme Fahd wa Kuchapisha Qur’ani Tukufu mjini Madina na hadi leo hii anaendelea na kazi hiyo. Kama tulivyotangulia kusema, kazi yake imechapishwa na kuenea katika kona zote za dunia.

Khati maarufu za Uthman Taha

Taarifa zinasema kwamba, licha ya kuwa na umahiri wa hali ya juu wa uandishi wa khati, lakini Uthman Taha kila siku ya Mungu huwa anafanya mazoezi ya kuandika khati za kila namna.

Miongoni mwa matamshi yake maarufu ni pale aliponukuliwa akisema, “Natamani aya zinazozungumzia pepo zisifikie mwisho.”

Miongoni mwa matamshi yake maarufu ni pale aliponukuliwa akisema:

“Natamani aya zinazozungumzia pepo zisifikie mwisho.”

Siku chache zilizopita, kulikuwa na taarifa kwamba Uthma Taha (86) amepatwa na kirusi cha COVID-19. Hata hivyo taarifa zilizotolewa baada ya kufanyiwa uchunguzi zimesema kuwa hajaambukizwa kirusi hicho na hivi sasa anaendelea na shughuli zake kulingana na hali inavyomruhusu ya kiafya baada ya kulazwa hospitalini kwa muda wa siku 13. Hayo ni kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Arab News.

(Visited 106 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!