Stephen Jackson, mchezaji maarufu wa zamani wa mpira wa vikapu katika ligi maarufu ya NBA ya Marekani, ametangaza kusilimu na kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu. Ametoa tangazo rasmi la kusilimu kwake katika mitandao ya kijamii.

Mtandao wa “About Islam” umeripoti habari hiyo kwa kumnukuu Jackson akiandika: “Alhamdulillah, leo ni katika siku bora kabisa katika maisha yangu. Ninawapenda wale wote ambao wanawapa zawadi wa upendo watu wote (bila ya ubaguzi).”

Vile vile amewashukukru marafiki zake waliompa taarifa mbalimbali kuhusu mafundisho matukufu ya Uislamu na wote waliomsaidia katika sherehe za kutangaza kwake rasmi kuwa amesilimu. Ameandika: “Leo naona fakhari kubwa sana kukutana na kuwa pamoja nanyi ndugu zangu.”

Vile vile Stephen Jackson ameweka mtandaoni kipande cha video wakati alipotamka shahada mbili na kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu tarehe 6 Januari 2021.

Mwanamichezo huyo maarufu mwenye umri wa miaka 42 amechezea timu kadhaa na kushiriki katika mashindano mengi ya Ligi ya Mabingwa ya NBA ya mpira wa vikapu huko Marekani. Mwaka 2003 alichukua kombe akiwa pamoja na timu ya San Antonio Spurs. Habari hiyo imewafurahisha mashabiki wake. Mmoja wa wachangiaji ambaye naye hivi karibuni ameingia katika dini tukufu ya Kiislamu ameandika, ninamuomba Mwenyezi Mungu atupe taufiki na atutie nguvu katika safari yetu hii mpya kwa nyoyo zilizo wazi na akili zilizoamka. Mwengine ameandika: “Karibu sana nyumbani. Mwenyezi Mungu humuongoa yeyote anayetaka kuongoka.”

(Visited 45 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!