Hatimaye Msikiti mkubwa zaidi barani Afrika na ambao ni wa tatu kwa ukubwa duniani umefunguliwa rasmi leo Jumatano, Oktoba 28, 2020 kwa kusaliwa Sala ya jamaa nchini Algeria.

Hayo yametangazwa na mtandao wa habari wa “Yahoo News” Msikiti mkubwa zaidi barani Afrika unaojulikana kwa jina la Djamaa El-Djazair umefunguliwa kwa mnasaba wa mwezi 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal, wakati wa maadhimisho ya Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW.

Msikiti huo umeakhirishwa  kufunguliwa rasmi kwa muda wa mwaka nzima kutokana na sababu mbalimbali. Hapa chini tumeweka baadhi ya picha za msikiti huo, kama ambavyo unaweza kutembelea makala ya Ujue Msikiti mkubwa zaidi Afrika, kwa maelezo zaidi.

(Visited 78 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!