Misikiti 12 iliyokuwa imefungwa kutokana na janga la corona imefunguliwa tena leo Jumapili, Agosti 23, 2020 katika mikoa ya Sanglang, Simpang Empat na Guar Sanji nchini Malaysia.

Mtandao wa habari wa Berna umeripoti habari hiyo na kumnukuu mfalme kijana wa jimbo la Perlis, Tuanku Sayyid Faizuddin Putra Jamalullail akisema kuwa uamuzi wa kufunguliwa tena misikiti hiyo utaruhusu Waislamu kufanya ibada na shughuli zao mbalimbali na kwamba Sala ya Adhuhuri ya leo Jumapili itaanza tena kusaliwa kwenye misikiti hiyo.

Hata hivyo amesema, Waislamu wanahimizwa kwa kusisitiza kwamba wachunge taratibu zote za kiafya kwani bado ugonjwa wa COVID-19 ungaliko nchini Malaysia.  

Kwa upande wake Tuanku Sayyid Faizuddin Putra ambaye ni mkuu wa Baraza la Waislamu la Malaysia (MAIPs) amesema kuwa, mipango mbalimbali imeandaliwa ya kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza ili nchi hiyo isije ikalazimika kuifunga tena misikiti hiyo kutokana na corona.

(Visited 43 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!