Raia mmoja wa Kuwait amepata umaarufu sana katika mitandao ya kijamii kwa kuweka bango la ramani ya ardhi ya Palestina mbele ya nyumba yake ikiwa ni kutangaza upinzani wake kwa hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuitambua rasmi Israel.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Palestina SWAFA, Muhammad Iwadh al Wasmi, raia wa Kuwait aliyezaliwa mwaka 1982 ambaye anaishi katika eneo la Swabah al Nasir la mkoa wa Al Farwaniyah wa mashariki mwa Kuwait amecnukua hatua hiyo kuonesha kuwa wananchi wa nchi za Kiarabu hawaungi mkono uhusiano baina ya nchi zao na Israel.
Hatua ya raia huyo wa Kuwait ya kubandika bango la ramani ya Palestina mbele ya nyumba yake imeakisiwa sana katika mitandao ya kijamii.
Alipohojiwa na Shirika la Habari la Palestina SWAFA, raia huyo wa Kuwait amesisitiza kuwa, msimamo wa asili wa serikali na wananchi wa Kuwait ni kuliunga mkono taifa la Palestina na kupoinga uhusiano na Israel. Amesema sisi tangu zamani tuna mapenzi makubwa na kadhia ya Palestina.
Aidha amesema, ameanzisha jambo hilo ili liwe kigezo kwa raia wengine wa Kuwait na nchi zote za Kiarabu na Kiislamu waweze kuonesha kwamba Waislamu hawaridhishwi na hatua ya baadhi ya nchi ya kutangaza uhusiano rasmi na Israel.