Watu kadhaa wanahofiwa kufa baada ya ndege ya mizigo kuanguka Sudan Kusini wakati ilipokuwa katika harakati za kuruka katika uwanja wa ndege wa Juba.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juba, Kur Kuol ameliambia shirika la habari la Anadolu kuwa, watu wanane walikuwemo kwenye ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la Sauth West Aviation na ilikuwa inaelekea katika jimbo la Bahr el Ghazal la kaskazini mwa nchi hiyo.

Kuol amesema watu wanane waliokuwemo kwenye ndege hiyo bado hawajulikani walipo.

Hata hivyo watu walioshuhudia wamesema kuwa wameona miili ya maiti sita na mtu mmoja akiwa amejeruhiwa na kuwahishwa hospitalini.

(Visited 13 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!