Msikiti wa Mir Muhammad Shah wa jimbo la Heyderabad, kusini mw India, ni moja ya Misikiti midogo zaidi inayojulikana duniani leo hii ingawa sasa hivi uko katika hatari kubwa ya kuporomoka.

Msikiti huo ambao umejengwa juu ya kilima, una ukubwa wa mitamraba 10 tu na uwezo wa kupokea watu watano tu kwa wakati mmoja.

Inaaminiwa kwamba Msikiti huo ulijengwa kwa amri ya mfalme Muhi-ud-Din Muhammad ambaye ni maarufu kwa jina la Aurangzeb. Alikuwa ni mfalme wa sita wa silisila ya wafalme wa Gorgan India au Mughal aliyetawala kuanzia mwaka 1067 hadi 1118 Milaadia.

Msikiti huo ambao ndio mdogo zaidi wa kale duniani, umejengwa kwa mawe. Una tao moja na minara miwili. Kama tulijivyosema, zaidi ya watu watano hawawezi kuingia kwa wakati mmoja Msikitini humo. Hata hivyo mazingira yaliyouzunguka Msikiti huo ni ya kuvutia.

Hapa chini tumeweka kipande kifupi cha video cha msikiti huo

Hapa chini tumeweka pia baadhi ya picha za Msikiti huo.

(Visited 137 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!