Baraza la Wakfu wa Kiislamu katika mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas huko Palestina, leo Jumatano limefikia uamuzi wa kusimamisha kutekelezwa ibada ya Sala katika Msikiti wa al Aqsa kwa muda wa wiki tatu kama njia ya kupambana na maambukizi ya kirusi cha corona.

Hayo yameripotiwa na gazeti la al Quds al Arabi ambalo limemnukuu Hatam Abdul Qadir, mjumbe wa baraza hilo akisema kwamba, wamefikia uamuzi wa kusimamisha kwa muda kuingia Waislamu na wafanya ziara ndani ya Msikiti wa al Aqsa kuanzia keshokutwa Ijumaa kwa muda wa wiki tatu kutokana na kuongezeka maambukizo ya COVID-19. Takwimu za mwisho zilizotangazwa na maafisa wa Wizara ya Afya ya Palestina zinaonesha kuwa, wakazi 8000 wa mji wa Quds wamepatwa na ugonjwa wa COVID-19 kuanzia mwezi Julai mwaka huu hadi hivi sasa huku wagonjwa 2000 kati ya hao wakiwa bado wanateseka kwa ugonjwa huo thakili.

(Visited 61 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!