Familia za wahanga wa kitendo cha kihalifu cha shirika moja la Ufaransa cha kuingiza damu chafu ya UKIMWI nchni Iraq zimetaka shirika hilo lishtakiwe kwa jinai yake hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la “al Ma’aluma,” familia za wahanga waliodungwa damu chafu ya UKIMWI iliyoingizwa na shirika la Ufaransa la Sanofi katika mkoa wa al Anbar, Iraq, jana Jumamosi ziliitaka serikali ya nchi hiyo kulifuatilia kisheria shirika hilo la Ufaransa kutokana na kusababisha vifo vya raia 230 wa Iraq.

Baba Muiraq aliyepoteza watoto wake 5 kwa kudungwa UKIMWI na shirika la Ufaransa la Sanofi, bado anapigania kutendewa uadilifu

Khalil Ibrahim al Dulaimi, mmoja wa wakazi wa mji wa Fallujah nchini Iraq ambaye ni miongoni mwa waliodungwa damu hiyo chafu ya UKIMWI amesema, hospitali za mafunzo ya watoto katika mikoa wa al Fallujah na al Ramadi zilishuhudia vifo vya ghafla vya watu tisa mwaka 1986 ambao walipoteza maisha baada ya kudungwa damu chafu iliyoingizwa nchini Iraq na shirika la Sanofi la Ufaransa. Uchunguzi ulionesha kuwa watu hao walidungwa sindano za damu zilizokuwa na virusi vya UKIMWI na kusababisha vifo vyao. 

 Al Dulaimi ameongeza kuwa, sindano hizo za damu ya UKIMWI walidungwa raia wengine wengi wa Iraq katika mikoa ya Karbala, Najaf, Basra, Baghdad na mikoa mingine kadhaa na kupelekea kufariki dunia zaidi ya raia 230 wa nchi hiyo ya Kiislamu. Watoto kadhaa na wafanyakazi pamoja na timu ya madaktari ni miongoni mwa wahanga wa jinai hiyo.

Suala la Waislamu wa Iraq kudungwa sindano za damu yenye virusi vya UKIMWI linahusiana na shirika la Ufaransa la Mérieux ambalo kazi yake ni kufanya utafiti wa dawa mbalimbali. Sasa hivi wahanga wa uhalifu huo wanaitaka serikali ya Iraq ifuatilie kisheria jinai hiyo.

(Visited 21 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!