Jina la msikiti huo ni Djamaa el Djazaïr (Kwa Kiarabu: جامع الجزائر‎). Ndio msikiti mkubwa zaidi barani Afrika na uko nchini Algeria.

Msikiti huo ndio wenye mnara mrefu zaidi duniani. Mnara wake una urefu wa mita 265 na hivyo kiujumla, jengo la msikiti huo ndilo refu zaidi barani Afrika

Eneo la ndani ya msikiti wa Djamaa el Djazaïr, msikiti mkubwa zaidi Afrika

Eneo la msikiti huo lina ukubwa wa mita mraba laki nne (400,000) na uko pembeni mwa Bahari ya Mediterranian. Ukumbi wa swala wa msikiti huo una uwezo wa kubeba waumini 37,000 kwa wakati mmoja.

Msikti huo wa Djamaa el Djazaïr huko Algeria ni jengo la tatu lililochukua eneo kubwa zaidi duniani. Limeupiku Msikiti wa Hassan II wa Casablanca wa nchini Morocco kwa ukubwa. Kabla ya hapo, msikiti huo wa Hassan II ndio uliokuwa mkubwa zaidi barani Afrika.

Muonekano mwingine wa msikiti wa Djamaa el Djazaïr

Kuna wakati ujenzi wa msikiti huo wa Algeria ulikwama kutokana na matatizo ya fedha baada ya kuporomoka bei ya mafuta katika soko la dunia. Wafanyakazi 2,300 kutoka ndani na nje ya Afrika wameshiriki katika ujenzi wa msikiti huo.

Uwanja wa msikiti huo wa Algeria una uwezo wa kubeba waumini 120,000 kwa wakati mmoja. Aidha msikiti huo una nafasi ya kuegesha magari 7,000.

Msikiti huo ulipangwa kufunguliwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani wa 1441 Hijria. Hata hivyo janga la COVID-19 lililazimisha kuakhirishwa ufunguzi wake. Sasa ufunguzi wa msikiti huo unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu wa 2020.

Msikiti mkubwa zaidi barani Afrika kwa kutokea juu

Jengo la msikiti huo lina madrasa kubwa ya Qur’ani, bustani, maktaba, nyumba za wafanyakazi, kituo cha zimamoto, jengo la makumbusho la sanaa za Kiislamu na kituo cha utafiti.

Msikiti huo umejengwa kwa uimara wa kuhimili tetemeko kubwa la ardhi hata la kiwango cha 9.0 kwa kipimo cha rishta. Ukumbi wake wa Sala una nguzo 618. Kuba la ukumbi wa Sala lina ukubwa wa futi 160 na urefu wa mita 70.

Hapa tumeweka video fupi baada ya ufunguzi wa msikiti huo

(Visited 195 times, 1 visits today)
3 thoughts on “Ujue msikiti mkubwa zaidi Afrika + Picha na Video”
  1. Woow Hata mimi ilikuwa sijuwi kuhusu huu msikiti InshaAllah nitajitahidi kuenda kuuwona kwa uwezi wa Allah. Shukran.

Leave a Reply to Nasra Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!