African Muslim Man Making Traditional Praying To God While Wearing A Traditional Cap Dishdasha

Waislamu mjini Durban Afrika Kusini wamepanga kulalamikia hukumu ya mahakama moja ya nchi hiyo ya kupiga marufuku kusomwa adhana katika msikiti mmoja mjini humo.

Mtandao wa habari wa “HeraldLive” umemnukuu wakili mmoja wa kituo cha Kiislamu mjini Durban akisema kuwa, wamepanga kukata rufaa Mahakama Kuu mjini humo kupinga hukumu ya kupigwa marufuku adhana katika msikiti wa kituo hicho.

Mwezi uliopita, Jaji Sidwell Mngani wa Mahakama Kuu ya Durban alisikiliza mashtaka ya mtu mmoja mwenye chuki na Uislamu na kupiga marufuku kusomwa adhana katika msikiti huo.

Mashtaka dhidi ya msikiti huo yalifunguliwa na Chandra Giri Ellaurie anayeishi jirani na msikiti huo akilalamika kuwa, kusomwa Adhana msikitini hapo kunalipa eneo lao sura ya Uislamu.

Baada ya kufunguliwa mashtaka hayo, jaji Mngani alikitaka kituo hicho cha Kiislamu kusoma adhana kwa namna ambayo haitosikika nje ya msikiti.

Mawakili wa kitu hicho cha Kiislamu wamesema kuwa, hukumu hiyo ya Jaji Mngani ni batili kwa sababu kadhaa na kwamba ni wajibu wa mahakama kutoa hukumu zake kiuadilifu na kwa kuzingatia maslahi ya wengi.

(Visited 16 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!