Kuanzia Jumatano ijayo ya Oktoba 7, 2020, misikiti 19 ya Singapore itaruhusiwa kuongeza maradufu idadi ya Waislamu wanaoshiriki kwenye Sala za Jamaa ikiwa ni sehemu ya mpango wa kufungua maeneo ya ibada yaliyofungwa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Hayo yamethibitishwa na Baraza la Waislamu la Singapore (MUIS) ambalo limeongeza kuwa, sasa misikiti hiyo itaruhusiwa kupokea Waislamu 100 kwa wakati mmoja kutoka Waislamu 50 waliokuwa wameruhusiwa katika hatua za awali.

Kutokana na kuweko idadi kubwa ya Waislamu wanaotaka kwenda misikitini huko Singapore, wakuu wa misikiti wameweka mfumo maalumu wa kusali kwa awamu na kuomba nafasi mapema msikitini kabla ya kwenda kwa ajili ya Sala.

Mfumo huo ulianza mwezi Juni mwaka huu wa 2020. Pamoja na hayo, idadi ya Waislamu waliojitokeza ni kubwa kiasi kwamba ililazimu kila Muislamu kupata nafasi nyingine ya kwenda kusali Msikitini baada ya kupita wiki saba za zamu yake iliyopita.

(Visited 16 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!