Wanafunzi 700 wa Qur’ani Tukufu, wa kike na wa kiume wanashiriki masomo ya viwango mbalimbali ya Qur’ani Tukufu kwa njia ya Intaneti nchini Saudi Arabia.
Hayo yameripotiwa na mtandao wa habari wa al Bad’i ambao umeongeza kuwa, masomo ya aya mbalimbali za Qur’ani Tukufu yameanzishwa katika mkoa wa ‘Rafaha’ wa kaskazini mwa Saudi Arabia na masomo hayo yanayoendeshwa kwa njia ya Intaneti yataendelea hadi mwezi 28 Mfunguo Tano, Safar mwaka huu wa 1442 Hijria.
Wanafunzi 700, wa kike na kiume wa nchini Saudi Arabia, kila siku usiku, baada ya Sala ya Magharibi wanashiriki kwenye masomo hayo kwa njia ya Intaneti ambayo yanajumuisha Hifdh na usomaji wa makhraj nzuri wa Qur’ani.
Lengo la kuanzishwa masomo hayo ni pamoja na kurekebisha utamkaji fasaha wa aya za Qur’ani Tukufu. Masomo hayo yanajumuisha usomaji na hifdhi ya juzuu za 1, 3, 5, 10, 15, 20 na 30.