Kuna madai kuwa, Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Kenneth Homer Bessent amehama nyumbani kwake na kwenda kujificha kwenye kambi ya kijeshi kwa kuhofia kuuliwa na Iran.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmael Baghaei ametoa majibu kuhusu madai yaliyoenea mitandaoni ya waziri wa Hazina wa Marekani kuhama nyumba na kwenda kujificha akiwaambia fiongozi wa Ikulu ya White House kwamba: “Hamuwezi kujivua na dhima ya uhalifu na jinai za kivita na vitendo vya kigaidi mlivyofanywa dhidi ya Iran kwa kutumia propaganda za vyombo vya habari na kujifanya wahanga na watu waliodhulumiwa.”
Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amegusia tuhuma mpya zinazoenezwa na viongozi wa Marekani na Israel za kuihusisha Tehran na vitendo vya kigaidi na kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba, uhalifu wa kivita uliofanywa na Israel na Marekani dhidi ya viongozi na wananchi wa Iran hauishii tu kuwa uhalifu wa kivita, bali pia ni ugaidi wa kiserikali wa kiwango cha juu mno uliojumuisha mauaji ya kigaidi ya viongozi na wanasayansi wa Iran pamoja na wanafunzi wa kike wa shule ya msingi.
Ameandika: “Hivi sasa Marekani imeanzisha propaganda kubwa ya vyombo vya habari chini ya anwani ya uongo ya kuihusisha Iran na ugaidi na kujionesha wao Wamarekani kuwa ni wahanga!”
Kuna taarifa zinazolinukuu gazeti la The New York Times la Marekani likiripoti mapema Jumatano kwamba Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, amehamishwa kutoka makazi yake na kupelekwa kwenye kambi ya kijeshi kutokana na hofu ya kuuliwa na Iran.
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: “Marekani ina dhana potofu kwamba, kwa kujifanya mhanga, dunia itasahau historia yake ndefu ya uvamizi na ugaidi; na kwa dhana yake hiyo potofu, Marekani inadhani kuwa itaifanya dunia iamini madai yake yasiyo na msingi…”
Amesema: Propaganda zinazochochewa na vyombo vya habari hauwezi kubadilisha ukweli wa kihistoria, wala kuwaondolea hatia wahalifu, wala kuwaficha wale waliofanya au kuamuru uvamizi wa kijeshi, ugaidi na jinai za kivita.
