Waziri wa Masuala ya Dini wa Tunisia amemuenzi na kumtunuku zawadi Maryam Uthmani, binti mdogo zaidi kuhifadhi Qur’ani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Watu mbalimbali muhimu wamehudhuria sherehe za kumuenzi “hafidha” huyo wa Qur’ani nzima zilizosimamiwa na Wizara ya Masuala ya Dini ya Tunisia akiwemo waziri mwenyewe, Ahmad Adhoum. Wazazi wawili wa binti huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 10, wameshiriki kwenye sherehe hizo ambazo zimefanyika maalumu kwa ajili ya kuenzi nafasi ya mama na kuhamasisha wazazi kuwalea KiQur’ani watoto wao. Sherehe hizo zimefanyika kwa mnasaba wa Siku ya Taifa ya Mwanamke, nchini Tunisia.
Maryam Uthmani ni mwenyeji wa mji wa Degache wa eneo la Djerid mkoani Tzeur, magharibi mwa Tunisia.
Awali Maryam alihifadhi nusu ya kwanza ya Msahafu na amemalizia nusu ya pili katika kipindi hiki cha karantini ya corona akisimamiwa ma ustadh wake bingwa wa fani ya hifdh.
Mbali na kupata taufiki ya kuhifadhi Qur’ani nzima akiwa bado mdogo, Maryam Uthmani ana kipaji kizuri pia katika hisabati na michezo.
Maashaallah Allah amhifadhi kijana wetu huyu
Aamin Ya Rabb