Idara ya Masuala ya Miongozo ya Kidini ya Saudi Arabia imeiwakilishi Idara Kuu ya Misahafu ya Nchi hiyo katika kuanzisha zoezi la kujiandikisha wanafunzi wa kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika Msikiti Mkuu wa Makka yaani Masjid al Haram.

Toleo la mtandaoni la gazeti la Sabq la Idara ya Miongozo ya Kidini ya Saudi Arabia limetangaza kuwa, uandikishaji wa wanafunzi wa Hifdh ya Qur’ani Tukufu katika Msikiti Mkuu wa Makka, umeanza kwa ajili ya msimu wa joto kali mwaka huu.

Ghazi bin Fahd, mkurugenzi wa Idara Kuu ya Masuala ya Misahafu ya Masjid al Haram amesema kuwa, masomo ya msimu wa joto ya kuhifadhi Qur’ani yatafanyika kuanzia mwezi 19 Mfunguo Mosi hadi mwezi 23 Mfunguo Pili 1442 Hijria kulingana na kalenda ya Saudi Arabia ambayo itasadifiana na tarehe Mosi Juni hadi tarehe 4 Julai, 2021.

Mkurugenzi huyo amesema, huu utakuwa ni mwaka wa pili mfululizo kufanyika masomo hayo kwa njia ya Intaneti. 

Pembeni mwa masomo ya Hifdh, wanafunzi wa masomo hayo wanafundishwa pia umuhimu wa kuwa na misimamo ya wastani na kujiepusha na misimamo mikali ambayo si katika mafundisho ya Uislamu. 

Ukurasa wa kujiandikisha wanafunzi unapatikana kwenye kiungo hiki: https://cutt.us/Mkhef

(Visited 167 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!