Msikiti wa kale wa makuba 9 ni moja ya majengo muhimu ya kihistoria nchini Bangladesh ambao una umri za karibu karne tatu au nne yaani miaka 300 hadi hadi 400.
Kwa mujibu wa The Financial Express, Msikiti huo uliojengwa karne kadhaa nyuma, uko katika eneo la Niamatpur Wilayani Naogaon magharibi mwa Bangladesh na unajulikana kienyeji kwa jina la Bhanga Masjid.
Msikiti huo wa ni wa ghorofa mbili na umejengwa juu ya nguzo nne kuu madhubuti. Msikiti huo una makuba tisa, minara minne katika pembe zake mnara mmoja kwenye mlango wa kuingilia.
Wenyeji wa eneo hilo wanalalamikia kupuuzwa jengo hilo la kihistoria ambalo ni kivutio muhimu si kwa Waislamu tu, lakini pia kwa wasio Waislamu na hasa watalii kutoka nje ya Bangladesh.
Jengine ambalo linalalamikiwa na wananchi Waislamu wa Bangladesh ni kwamba, eneo hilo lina historia ndefu na ni hazina na tunu muhimu ya kihistoria, lakini hadi hivi sasa Serikali imeshindwa kuuingiza Msikiti huo katika orodha ya turathi za kihistoria.
Waislamu hao wanalalamika pia kwamba Msikiti huo umetelekezwa katika miaka ya hivi karibuni na hata kukaribia kubomoka.