Wazazi nchini Brunei Darussalam wameelezea kufurahishwa sana na uamuzi wa kufunguliwa upya masomo ya Qur’ani katika kituo cha Jame’ ‘Asr Hassanil Bolkiah baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kutokana na janga la COVID-19.
Taarifa iliyoripotiwa na Bormeo Bulletin inasema kuwa, wazazi nchini Brunei wamefurahi sana kuona sasa watoto wao wanaweza kujaza muda wao wa faragha wakiwa madrasa wanapomaliza masomo yao shuleni. Wazazi hao wamesema wana uhakika kwamba serikali itachukua hatua zote za lazima za kuzuia kuenea kirusi cha corona.
Mmoja wa maafisa wa masuala ya Qur’ani nchini Brunei, Imam Abdul Aziz bin Haji Abdullah amesema kuwa, masomo ya Qur’an yalianza rasmi Ijumaa iliyopita na yanafanyika kwa mujibu wa maelekezo ya watu wa afya na ushauri wa Idara ya Masuala ya Misikiti ya nchi hiyo. Amesisitiza kuwa, kuchungwa masuala ya afya ndani na nje ya maeneo ya madrasa ni muhimu sana katika kukabiliana na maambukizo ya corona.