Baraza la Uhusiano na Marekani na Uislamu jana Jumamosi lilijiunga na asasi za eneo la Joplin kumtaka Mkuu wa Kaunti ya Jasper, John Bartosh ajiuzulu baada ya kupata jumbe zake alizozituma mtandaoni mwaka 2019 ambazo taasisi hiyo inaamini ni za kueneza chuki dhidi ya Uislamu.
Katika moja ya ujumbe wake alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Bartosh alipendekeza kwamba misikiti yote nchini Marekani izingirwe na bar za mabaradhuli, wanawake wanaokaa uchi wa mnyama, bucha na mikawaha ya nguruwe, maduka ya pombe na mambo mengine machafu ambayo ni haramu kwa Waislamu. Itambulike kwamba ni haramu kwa Waislamu kunywa pombe na kula nyama ya nguruwe au chochote kinachotokana na nguruwe. Ujumbe wa Mkuu huyo wa Kaunti ya Jasper huko Marekani ulitaja pia kwa uchache jina moja la duka la vitu ambavyo ni haramu kwa Waislamu.
Katika ujumbe wake mwingine, Bratosh alisema: ”Denmark imepiga marufuku burqa. Waambie Waislamu wabadilishe utamaduni wao, wafaidike na sheria au waondoke nchini.”
Taasisi hizo za Kiislamu aidha zimekasirishwa sana na kitendo cha mtoto wa kiume wa miaka 16 wa mkuu huyo wa Kaunti ya Jasper huko Marekani ambaye ameonekana katika video iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii akiwa na chupa ya bia mkononi huku akiimba nyimbo za ubaguzi wa rangi. Bartosh ameomba radhi kwa kitendo hicho cha mwanawe na kusema mwanawe huyo hatoachwa vivi hivi bila ya kupewa adhabu.