Shirika la kimataifa la Human Rights Watch limetoa ripoti maalumu na kufichua mateso wanayoyapata Waislamu wa jamii ya Rohingya katika kambi za wakimbizi za eneo la Rakhine la magharibi mwa Myanmar na jinsi uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu na unyanyasaji wa Waislamu unavyofanyika kwenye kambi hizo.

Shirika la habari la Anadolu limenukuu ripoti ya shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch likisema, wanajeshi wa Myanmar wanawatia mbaroni Waislamu wa jamii ya Rohingya kiholela, bila ya kikomo, tena kwa umati.

Limesisitiza kuwa, karibu Waislamu laki moja na 30,000 wa jamii ya Rohingya wako katika kambi za wakimbizi huko Rakhine, magharibi mwa Myanmar tangu mwaka 2012 kutokana na ukandamizaji na ukatili wa kuangamiza kizazi wanaofanyiwa na wanajeshi wa nchi hiyo.

“Waislamu wanaishi katika mazingira ya kikatili na magumu sana kwenye kambi hizo za wakimbizi na hii ni moja ya jinai za kibinadamu na kuwanyima Waislamu hao haki zao za kimsingi kabisa kama vile uhuru wao,” imeongeza ripoti ya Human Rights Watch.

Duru za kieneo na za kimataifa zimeripoti kuwa, jinai kubwa wanazoendelea kufanyiwa Waislamu wa jamii ya Rohingya huko Myanmar (Burma) kunakofanywa na wanajeshi na wanamgambo wa kibudha zimeshaua maelfu ya Waislamu na kuwafanya wakimbizi mamia ya maelfu ya wengine, huku milioni nzima wakiishi katika mazingira magumu na duni mno kwenye kambi za wakimbizi katika nchi jirani ya Bangladesh.

(Visited 42 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!