Shirikisho la Waislamu wa New Jersey limeanza kujenga Msikiti mpya wa kuweza kukidhi ongezeko la Waislamu katika jimbo hilo la kaskazini mashariki mwa Marekani.

Mtandao wa “NJ -True Jersey” umeripoti habari hiyo na kulinukuu Shirikisho la Waislamu wa Jew Jersey ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali yenye makao yake Jersey City ikisema kwamba, ujenzi wa Msikiti huo mpya ambao utakuwa wa ghorofa mbili, kuba moja na mnara mmoja umeanza katikati ya jiji hilo.

Mradi huo utajumuisha pia ujenzi wa maduka makubwa na sehemu za kuegeshea magari.

Arshad Chatha, Mkuu wa Shirikisho la Waislamu wa New Jersey amesema, jamii ya Waislamu katika jimbo hilo inazidi kuwa kubwa, hivyo wanahitaji kuwa na sehemu kubwa zaidi ya kufanyia ibada na shughuli zao nyinginezo, sehemu ambayo mbali na mvuto wake wa kiroho na kimaanawi, inapaswa iwe na mvuto mkubwa pia wa usanifu majengo na hadhi inayokubalika.

Amesema kuanza mradi huo ni ushahidi kwamba idadi ya Waislamu huko New Jersey inazidi kuwa kubwa.

Amesema, tangu ashike uongozi wa Shirikisho la Waislamu wa New Jersey katika muongo wa 1980, idadi ya Waislamu katika jimbo hilo la Marekani imeongezeka mara tatu. Anasema, wakati aliposhika uongozi wa shirikisho hilo, familia za Waislamu zilikuwa zikisali Sala za jamaa kwa kukusanyika kwa zamu katika nyumba zao.

(Visited 63 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!