Jaji mmoja nchini Canada ambaye miaka mitano iliyopita alikataa kusikiliza kesi ya mwanamke Muislamu kutokana na kwamba amevaa vazi la staha ya Kiislamu la Hijab, hatimaye ameomba radhi baada ya kupita miaka mitano.

Shirika la habari la Anadolu limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mwaka 2015, Jaji Eliana Marengo wa jimbo la Quebec huko Canada, alikataa kusikiliza kesi ya Bi Rania el Alloul, Muislamu anayechunga vazi la staha la Hijab kwa madai kuwa vazi hilo haliruhusiwi kuingia mahakamani. Alishurutisha Muislamu huyo avue Hijab yake kama anataka kesi yake isikilizwe kuhusu kukamatwa gari yake.

Hatimaye jana Jumanne, Jaji Eliana alikiri kwamba alifanya makosa kumtaka Bi Rania avue Hijab kabla ya kuingia mahakamani. Jaji huyo amedai kuwa, alifananisha vazi hilo na heti na miwani ya jua, mavazi ambayo si ruhusa kuingia nayo mahakamani.

Akijibu ombi la msamaha la jaji huyo, Bi Rania amesema, nimekubali ombi lake kwani hivi ndivyo dini yangu tukufu ya Kiislamu ilivyonilea na kunifunza.

(Visited 65 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!