Waislamu nchini India wanaendelea na mpango wao wa kujenga hosptali ya kutoa huduma za kila namna pembeni mwa msikiti katika kijiji cha Dhannipur cha eneo la Ayodhya huko Uttar Pradesh.

Mtandao wa habari wa “Hindustani Times” umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Taasisi ya Utamaduni wa Kiislamu-Kihindi (IICF) imetangaza kuwa, hospitali hiyo inayojengwa pembeni mwa msikiti, itakuwa na vitanda 200 vya wagonjwa na itakuwa inatoa huduma zote za matibabu.

Si hayo tu, eneo hilo litakuwa pia na sehemu ya makumbusho, maktaba na hata eneo la kupikia la utamaduni wa Waislamu wa India.

Eneo hilo ni lile ambalo Waislamu wamepewa na Serikali baada ya Mabaniani na Wahindu wanaochukia Uislamu, kuuvamia msikiti wa Babri, kuuvunja na sehemu yake kujenga maabadi yao kwa madai ya uongo ya eti eneo hilo alizaliwa mungu wao.

At’har Hussein, msemaji wa taasisi ya IICF amesema, hospitali hiyo itakuwa jengo kubwa zaidi la umma la jamii ya Waislamu wa India. Hata hivyo amesema, jina la hospitali hiyo halijafikiwa maamuzi ya mwisho. Ujenzi wa msikiti huo unatarajiwa kuanza rasmi miezi miwili ijayo.

Takwimu zinaonesha kuwa, kuna zaidi ya Waislamu milioni 172 nchini India. Waislamu ni wa pili kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu nchini India.

(Visited 12 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!