Serikali ya Kuwait imetangaza mafuruku ya kuingiza Misahafu na nakala za Qur’ani Tukufu nchini humo bila ya kibali rasmi cha Idara Kuu ya Kusimamia Uchapishaji na Usambazaji wa Qur’ani Tukufu.

Gazeti la al Watan limetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, Idara ya Ushuru ya kuwait imepokonywa ruhusa ya kuingiza nchini humo, nakala yoyote ya Qur’ani Tukufu bila ya kupata kwanza kibali rasmi kutoka kwa Idara Kuu ya Kusimamia Uchapishaji na Usambazaji wa Qur’ani Tukufu.

Sehemu moja ya tangazo hilo inasema, sheria iliyoasisi Idara Kuu ya Kusimamia Uchapishaji na Usambazaji wa Qur’ani Tukufu ya Kuwait inasema kuwa, ni marufuku kwa kiongozi yeyote wa kiserikali au wa kiraia au taasisi yoyote ile kuchapisha nakala yoyote ya Qur’ani Tukufu ndani na nje ya Kuwait bila ya kibali cha idara hiyo.

Kwa mujibu wa tangazo hilo jipya, yeyote atakayekwenda kinyume na amri hiyo atapigwa faini ya fedha taslimu zisizopungua Dinari 3000 za Kuwait na zisizopuindukia Dinari 5000. Kiwanda chochote kitakachokwenda kinyume na sheria hiyo mpya kitafungwa kwa muda usiopungua miezi mitatu.

(Visited 18 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!