Maandalizi ya kuwapokea Waislamu wafanya Umra na Ziara yanaendelea katika miji mitakatifu ya Makkah na Madina.
Vyombo mbalimbali vya habari vimeakisi habari hiyo na kuunukuu uongozi wa masuala ya Masjidul Haram nchini Saudi Arabia ukisema kwamba Nyumba ya Allah (Msikiti Mtakatifu wa Makkah) huwa unapigwa dawa mara 10 kila siku kama sehemu ya kukabiliana na maambukizo ya COVID-19. Wafanyakazi 450 ndio wanaofanya kazi hiyo ambayo inafanyika masaa 24 kila siku. Mazulia ya msikiti huo nayo yanasafishwa muda wote.
Hapa chini tumeweka baadhi ya picha ya maandalizi ya ibada hiyo ya Umra katika Msikiti Mtukufu wa Makkah.
(Visited 1 times, 1 visits today)