Waziri Mkuu wa Misri ametangaza kuafikiana na mpango wa kufanyika Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Qur’ani huko Port Said, Misri.
Kwa mujibu wa Al-Mal News, Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly amesema anaafiki kufanyika mashindano ya sita ya kimataifa ya Qur’ani katika mji wa Port Said wa kaskazini mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Mashindano haya yatafanyika katika jimbo la Port Said kwa ushirikiano wa Shirika la Kitaifa la Vyombo vya Habari na kwa msaada wa Meja Jenerali Adel Barihan, gavana wa Port Said.
Adel Moslehi, mwanzilishi na mratibu wa shindano hayo, amesema: Meja Jenerali Ghadban tayari ameanza kuchukua hatua maalumu za kufanikisha mashindano hayo.
Aliomba Kamati Kuu kufanya haraka kuitisha mashindano ya mchujo kwa ajili ya kuchagua wawakilishi wa Misri katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu.
Moslehi ameongeza: Mashindano ya mara hii yamepewa jina la marehemu Sheikh Nasreddin Tobar na yamepangwa kufanyika Februari 17 mwakani katika fani nne.
Kamati Kuu ya Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu ya huko Port Said imeamua kushiriki katika mashindano hayo ya sita chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu Mostafa Madbouly katika sehemu zifuatazo:
Sehemu ya kwanza: kuhifadhi Qur’ani Tukufu nzima kwa kisomo kamili, kwa mfano qiraa ya Imam Asim na riwaya za Shuba na Hafs, au kisomo cha Imam Nafee kwa riwaya za Qalun na Warsh, au kisomo chochote katika ya visomo kumi vya Qur’ani Tukufu.
Sehemu ya pili: sauti nzuri na usomaji bora unaochunga kikamilifu sheria zote za usomaji.
Sehemu ya tatu: kuhifadhi Qur’ani Tukufu nzima kwa riwaya moja (maalumu kwa ajili ya mashindano ya wanawake) kwa kuchungua kikamilifu sheria za usomaji.
Sehemu ya nne: Dua na Kasida.
Moja ya masharti yaliyowekwa ya kushiriki katika mashindano hayo ni kwamba mshiriki lazima awe kwa uchache na umri wa miaka 16 na asipindukie miaka 30. Aidha, kila mshiriki anaruhusiwa kushiriki katika sehemu moja tu.
Washindi wote wa mashindano yaliyopita ya ya kimataifa hawatoshiriki kwenye mashanidano ya mara hii. Washiriki wanaweza kujiandikisha kupitia b-pepe hii: alfaezoun.portsaid@gmail.com
Kila mmoja wa washiriki lazima atume sauti ya dakika tatu kupitia barua pepe hiyo. Zaidi ya hayo, lazima pia atoa maelezo kamili ya kujitambulisha, ikiwa ni pamoja na jina, umri, anwani, nambari ya simu, na uwanja ambao anataka kushiriki.
Tarehe 10 Oktoba 2022 ndiyo siku ya mwisho ya kushiriki katika mashindano hayo.