Awamu ya pili ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu yaliyopewa jina la “Qarii wa Dunia wa Quds” imefanyika katika mji wa Baytul Muqaddas kwa hima ya kikundi kimoja cha vijana wa Palestina.

Mtandao wa habari wa Dar al Hayat umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, kikundi cha Huna al Quds cha vijana wa Palestina wa mji wa Baytul Muqaddas kimetangaza kuanza mchakato wa mashindano hayo.

Washiriki walianza kujiandikisha mwezi 27 Rajab kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Miiraj; siku ya Ijumaa na yatamalizika mwezi 10 Ramadhani. Matokeo ya mashindano hayo yatatangazwa mwezi 25 mwezi huo huowa Ramadhani mwaka huu wa 1442 Hijria na washindi watapewa zawadi nono pamoja na loho na nishani maalumu ya pongezi.

Kikundi hicho cha vijana wa Palestina kimetumia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Facebook na pia tovuti yake ya Huna al Quds kuwaomba maqarii wote popote walipo duniani washiriki katika mashindano hayo ya kimataifa kwa njia ya Intaneti.

Ni vyema tukasema hapa kwamba, awamu ya kwanza ya mashindao ya Qur’ani Tukufu kwa jina hilo yaliitishwa na kikundi hicho cha Huna al Quds mwaka 2016 Milaadia. Washiriki 850 kutoka pembe zote za dunia walishiriki katika mashindano hayo. Jopo la majaji walipitia kwa kina visomo vyote vya tajwidi walivyotumiwa kwa njia ya Intaneti na kuchagua maqarii 10 wa kuingia daraja nyingine.

Huna al Quds ni kikundi cha vijana wa Palestina wanaoshi katika mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas wenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa. Kikundi hicho kinafanya harakati nyingi za kuulinda mji huo mtakatifu zikiwemo za kielimu na kiutamaduni.

(Visited 47 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!