Kituo kimoja cha elimu cha Waislamu nchini Marekani cha Msikiti wa San Antonio katika jimbo la Texas kimewekwa maalumu kwa ajili ya kutoa huduma bure ya vipimo vya corona kutokana na utulivu na usalama wake.

Mtandao wa habari wa “News4SA” umeripoti habari hiyo na kunukuu taarifa iliyotolewa na Sakib Shaikh, Msemaji wa Kituo cha Elimu ya Watoto na Huduma za Jamii cha Waislamu katika mji wa San Antonio iliyosema kwamba, kituo hicho kimeamua kutoa huduma ya bure ya vipimo vya COVID-19.

Alipoulizwa sababu ya kuchukuliwa uamuzi huo amesema, Msikiti ni eneo ambalo linawapa Waislamu utulivu wa kipekee.

Aidha amesema, tunajua kwamba ziko sehemu nyingine ambazo tungeliweza kuzitenga kwa ajili ya kuchukulia vipimo vya corona, lakini tumeona ni vizuri Waislamu wakachukulia vipimo hivyo katika eneo ambalo linawapa utulivu wa kipekee na kujihisi wako katika amani kabisa. Sehemu hiyo si nyingine isipokuwa Msikitini. Zoezi hilo limepangwa kufanyika tarehe 17 mwezi huu wa Agosti 2020. Litaanza saa tano asubuhi na kuendelea hadi saa tisa mchana. Zoezi hilo litafanyika ndani ya gari.

(Visited 22 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!