Licha ya ugonjwa wa corona kuendelea kuiathiri sana dunia wakiwemo Waislamu na ibada zao, lakini mwezi mtukufu wa Ramadhani haukuzuiwa na ugonjwa huo kung’arisha nuru yake ya watu kupendana na kusaidiana katika kona mbalimbali duniani.

Ratiba za ibada katika maeneo mengi zimeathiriwa na COVID-19 lakini pamoja na hayo shauku, mapenzi na ukarimu wa Waislamu unaonekana waziwazi. Hapa chini tumeweka baadhi ya picha za baadhi ya maeneo ya Waislamu duniani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani wa 1442 Hijria. Zinavutia kuziangalia.

Waislamu wa India wakiwa kwenye futari katika siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani 1442 Hijria katika eneo la kale la New Delhi.

Waislamu wakiomba dua kabla ya kula futari katika Msikiti wa Lahore, Pakistan kwenye Ramadhani ya mwaka 1442 Hijria
Waislamu wakiomba dua kabla ya futari katika Msikiti mmoja huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistan.
Waislamu wa Lahore, Pakistan wakinunua futari katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani wa 1442 Hijria.
Wafanya ibada ya Umra wakitufu AlKaaba huko Makkah, Saudi Arabia katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani 1442 Hijria.
Waislamu wa Oman katika maandalizi ya Ramadhani ya 1442 Hijria (2021). Picha na Gulf News
Waislamu wa Palestina wakijiandaa kula futari katika eneo la kale la mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas tarehe 13 Aprili 2021.
Dua ya Waislamu wa Indonesia muda mchache kabla ya futari katika Msikiti mmoja kaskazini mwa Sumatra.
Ibada ya kusoma Qur’ani pia inaendelea wakati huu wa Ramadhani. Hapa ni katika Msikiti Mkuu wa mji wa New Delhi, India.
Wakati wa kukaribia futari karibu na Msikiti wa Sultan Ahmad maarufu kwa jina la Msikiti Buluu nchini Uturuki. Msikiti huo umepambwa kwa fanusi na taa za Ramadhani katika eneo la kihistoria la Sultan Ahmad, mjini Istanbul, tarehe 13 Aprili, 2021.
(Visited 217 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!