Waislamu mjini Makka wametekeleza ibada ya Sala ya Ijumaa kwa kuchunga taratibu na miongozo yote ya watu wa afya kwa ajili ya kujiepusha na maambukizo ya COVID-19.
Mamlaka ya kusimamia Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina imechukua hatua zote za usafi hata wa kwenye vipaza sauti kama ilivyoagizwa na watu wa afya.
Khutba za Ijumaa za Msikiti wa Makka zimetarjumiwa kwa lugha mbalimbali kwa ajili ya Waislamu wa maeneo tofauti.
Wanachuo 80 wa dini mjini Makka wanajitolea kutoa huduma kwenye Msikiti huo mtakatifu kwa wastani wa masaa matano kila siku. Hapa chini tumeweka baadhi ya picha za Sala ya Ijumaa katika Msikiti Mtakatifu wa Makka.
(Visited 242 times, 1 visits today)