Sherehe za mwaka wa 12 wa tangu kufunguliwa Bustani ya Qur’ani nchini Qatar zimefanyika lakini kwa njia ya Intaneti kutokana na kuenea ugonjwa wa COVID-19. Bustani hiyo ni ya Taasisi ya Elimu, Sayansi na Ustawi wa Jamii ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa al Sharq wa Qatar, sherehe hizo zimerusha hewani mubashara video za maeneo tofauti ya Bustani hiyo ya Qur’ani, mimea mbalimbali na makumbusho ya mimea pamoja na eneo la kuhifadhia mimea.

Sherehe hizo zimetumika kuonesha jinsi Uislamu unavyolipa umuhimu mkubwa suala la kulindwa mazingira kama ambavyo zimetumika pia kuonesha kazi mbalimbali zinazofanywa na asasi ya bustani hiyo.

Vile vile sherehe hizo zimetumika kufanya kampeni ya kupanda miti 2022 na kusisitiza kwamba taasisi ya Bustani ya mimea iliyotajwa katika Qur’ani Tukufu ndiyo itakayosimamia kampeni hiyo. Kwa mujibu wa taarifa, hadi hivi sasa mimea elfu mbili imeshapandwa. Miongoni mwa shabaha kubwa za Bustani ya Mimea Iliyotajwa katika Qur’ani ni kuwakumbusha walimwengu wajibu wao wa kulinda vizuri mazingira na pia kuwahamasisha watu wa rika na makundi tofauti hasa wanafunzi kujenga utamaduni wa kuwa na bustari katika maeneo wanayoishi ili kutekeleza vizuri mafundisho ya Uislamu ya kulinda mazingira.

(Visited 47 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!