Taasisi Kuu ya kijamii ya Kiislamu nchini Marekani inayojulikana kwa kifupi CAIR imemshutumu Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na serikali yake kwa kutoa “makataa” na muda maalumu kwa Waislamu wa nchi hiyo kuhakikisha wanaachana na mafundisho ya dini yao na kujivika utamaduni wa Magharibi.

Hayo yameripotiwa na Middle East Eye na kusema kwamba baada ya matamshi ya siku ya Jumatano ya Emanuel Macron kwa Baraza la Waislamu wa Ufaransa (CFCM) ambaye aliwapa Waislamu “makataa” na muda wa siku 15 kuhakikisha wanajivika utamaduni wa Magharibi, Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR) limemshutumu vikali Macron na kulaani kitendo chake hicho. Limesema, serikali ya Ufaransa haina haki ya kuwalazimisha Waislamu au watu wengine wowote wa jamii za wachache, kuachana na imani zao na kufuata tamaduni ambazo ni kinyume na itikadi zao wala kuwalazimisha kufasiri mafundisho ya dini yao kwa mujibu wa wanavyotaka Wamagharibi.

Macron ameitaka taasisi hiyo ya Kiislamu kusaini hati maalumu ya kujivika utamaduni wa Magharibi. Hati hiyo aidha inapiga marufuku kujihusisha wageni na masuala ya misikiti nchini Ufaransa kama ambavyo sheria hiyo mpya itaunda Baraza la Taifa la Maimamu wa Misikiti ili kuwadhibiti Waislamu. Tamko wa taasisi kubwa zaidi ya kiajamii ya Kiislamu nchini Marekani CAIR limesema, katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, Ufaransa imetekeleza sheria nyingi za kuwadhibiti na kutoa adhabu kwa Waislamu kiasi kwamba hata kuvaa nguo za staha ya mwanamke wa Kiislamu yaani Hijab kumepigwa marufuku maskulini na makazini kwa wanafunzi, walimu na wafanyakazi Waislamu wa taasisi za serikali.

(Visited 25 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!