Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Utalii wa Halali nchini Uturuki amesema kuwa, idadi ya watalii wa sekta hiyo inayochunga mafundisho yote ya kiislamu, imeongezeka sana nchini humo katika kipindi hiki cha ugonjwa wa corona au COVID-19.

Hayo yameripotiwa na mtandao wa habari wa Turk Press ambao umemnukuu Emrullah Ahmet Turhan akisisitiza kuwa, idadi ya watu waliofanya utalii wa Halali katika kipindi hiki cha corona ni kubwa ndani ya Uturuki.

Ameliambia shirika la habari la Anadolu kuwa, ongezeko la watalii katika sekta ya Halali ni kubwa kiasi ambacho hata jumuiya hiyo haikutarajia kujitokeza kiwango hicho kikubwa cha watalii katika sekta hiyo. 

Ameongeza kuwa, kuna ongezeko la asilimia mia moja ya watu waliotoa oda ya kuwekewa nafasi za vyumba katika hoteli zenye villa maalumu, na hii ni mara ya kwanza kujitokeza idadi kubwa kiasi hicho cha watalii kwani katika miaka ya kabla ya COVID-19, maombi ya nafasi za vyumba yalikuwa ni kwa asilimia 90 hadi 95 katika sekta ya utalii Halali.

Vile vile amesema, kustawi sekta ya utalii wa Halali kumetanua wigo wa biashara kwenye sekta hiyo na matokeo yake ni kuongezeka uwekezaji katika utalii wa Halali.

(Visited 41 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!