Licha ya Somalia kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 1991 hadi hivi sasa, lakini usomeshaji wa Qur’ani ikiwemo hifdh unaendelea. Si kazi rahisi kuendelea na usomeshaji huo, lakini mapenzi makubwa ya Waislamu kwa Kitabu Kitakatifu cha Qur’ani yanawafanya wasikwamishwe na chochote katika kuwasomesha watoto wao na kujibidiisha wao wenyewe kukisoma na kukihifadhi kwa moyo.

Mashirika ya habari ya ndani ya Somalia yanaripoti kuendelea usomeshaji wa Qur’ani Tukufu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo licha ya kwamba imo kwenye lindi la umaskini, vita, na mashambulizi ya mara kwa mara ya ndani.

Mbinu kuu inayotumiwa na vyuo vingi vya Somalia katika kuhifadhisha Qur’ani tukufu, ni ile ile mbinu ya kale, lakini inaonekana inasaidia sana. Ni mbinu ya kutumia loho za mbao au hata za mawe kuandika na kufuta aya za Qur’ani Tukufu.

Watoto wa umri wa chini hadi miaka 18 wanatumia fursa ya umri wao kuhifadhi Qur’ani kupitia mbinu hiyo ya kuandika na kufuta hadi aya za Qur’ani zinajikita ndani ya nyoyo zao.

Walimu wanakuwa na nafasi ya kuwasikiliza watoto hao mara kwa mara kuona maendeleo yao ya hifdh na makhraj ya sauti zao.

Kipande cha video cha hapa chini ni sehemu ndogo ya mbinu inayotumiwa nchini Somalia, kuhifadhisha Qur’ani Tukufu.

(Visited 69 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!