Video inayomuonesha Waziri Mkuu wa Malaysia, Muhyiddin bin Haji Muhammad Yassin akisoma Qur’ani na mkewe imeenea sana katika mitandao ya kijamii, suala ambalo linaonesha wananchi wengi wa nchi za Kiislamu wana hamu ya kuona viongozi wao wanaitanguliza mbele Qur’ani Tukufu.
Mtandao wa lugha ya Kiarabu wa televisheni ya Al Jazeera umenukuu video hiyo iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii inayomuonesha Waziri Mkuu wa Malaysia, Muhyiddin bin Haji Muhammad Yassin akiwa amekaa kitako chini akisoma Qur’ani na familia yake akiwemo mkewe na kuonesha jinsi jambo hilo lilivyopokewa vizuri na watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Hata Balozi wa Qatar nchini Malaysia, Fahad bin Mohammed Kafood naye ameiweka video hiyo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ikiwa na maelezo yasemayo, Waziri Mkuu wa Malaysia, Muhyiddin Yassin akisoma Surat al Waaqiah na mkewe. Amma mwanasiasa kijana wa Malaysia, Ahmad Ismail naye ameweka video hiyo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na kuomba dua akisema: Ewe Mola wetu, muhifadhi kiongozi wetu, mpe uzima, nguvu, mafanikio na uongofu aweze kuiongoza vizuri nchi yake ya Malaysia.
Hapa chini tumeweka video hiyo inayomuonesha Waziri Mkuu wa Malaysia akisoma Qur’ani Tukufu na mkewe: