Mahakama ya mji wa Malerkotla huko Punjab nchini India, imewahukumu kifungo jela maadui wawili wa Uislamu walioivunjia heshima Qur’ani Tukufu.

Mtando wa habari wa Tribune of India umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mahakama ya mji wa Malerkotla imewapata na hatia watuhumiwa wawili kati ya wanne waliofunguliwa mashtaka ya kukivunjia heshima Kitabu kitakatifu cha Waislamu yaani Qur’ani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watuhumiwa wawili ambao hawakupatikana na hatia ni pamoja na Naresh Yadav, mkuu wa chama cha Aam Aadmi Party kwa kifupi AAP. Watuhumiwa wengine wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, kuazirishwa na kulipa faini ya Rupia 11,000.

Tarehe 24 Juni 2016, polisi wa India waliwatia mbaroni watu watatu baada ya kupatikana kurasa za Qur’ani Tukufu zikiwa zimechanwa na kutupwa barabarani katika mji wa Malerkotla wa jimbo la Punjab.

Siku chache baadaye, yaani tarehe 27 Juni 2016, mmoja wa watuhumiwa hao anayejulikana kwa jina la Vijay Kumar alikiri kwamba alishiriki katika kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu kwa amri ya Naresh Yadav, mkuu wa chama cha AAP. Polisi walianza uchunguzi wa kumsaili na kumfuatilia Yadav baada ya Vijay Kumar kudai alitumwa kufanya hivyo na mkuu huyo wa chama cha AAP. Mtuhumiwa wa pili aliyepatikana na hatia na kupewa adhabu hiyo ni Gaurav Kumar. Hata hivyo tarehe 13 Septemba 2018, Yadav aliomba kufanyike uchunguzi kuhusu kuingizwa fedha katika hesabu ya benki ya Kumar na uhusiano wake na genge la Rashtriya Swayamsevak Sangh kwa kifupi RSS. Genge hilo ni la wanamgambo wenye chuki na Uislamu na ni sehemu ya chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP) cha Waziri Mkuu Narendra Modi ambaye baada ya kuingia madarakani, chuki dhidi ya Waislamu zimeongezeka sana huko India.

(Visited 17 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!