Wawakilishi wa serikali ya Thailand ambao wamekwenda kusini mwa nchi hiyo kufanya mazungumzo na Waislamu wamesema kwamba pendekezo lililotolewa na Waislamu wa maeneo hayo ni kutaka siku ya Ijumaa iwe ya mapumziko rasmi nchini humo na sheria za Kiislamu zitawale katika mikoa minne ya kusini.

Mtandao wa habari wa “Bankok Post” umemnukuu Jenerali Wallop Raksanoh anayengoza timu ya wafanya mazungumzo kutoka serikalini akisema, wawakilishi wa Waislamu wametaka siku ya Ijumaa iitangazwe na katiba ya nchi hiyo kuwa siku rasmi ya mapumziko ili kuwapa fursa Waislamu kutekeleza ibada zao kwa uhuru hasa Sala za Ijumaa.

Waislamu hao aidha wameitaka serikali ya Thailand kuitangaza lugha ya Maleyu kuwa lugha rasmi katika mikoa ya Pattani, Yala, Narathiwat na Songkhla inayopakana na Malaysia huko kusini mwa Thailand.

Waislamu hao aidha wametaka watu wenye welewa wa masuala ya dini ndio wawekwe kushughulikia masuala ya Hija, kuandaa sheria za Kiislamu katika mikoa hiyo minne na kustawishwa sekta ya vyakula vya halali.

(Visited 33 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!