Waislamu nchini Sweden wanaendesha kampeni za kupambana na sheria za nchi hiyo ambazo zinaruhusu kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini.

Hatua hiyo ya Waislamu wa Sweden imechukuliwa baada ya adui wa Uislamu, Rasmus Paludan, raia wa Denmark kuanzisha kampeni ya kuchoma moto nakala za Qur’ani nchini Sweden. Jumuiya 15 za Waislamu nchini humo zimeitaka nchi hiyo kufanyia marekebisho sheria zake na kutoruhusu kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini. Waislamu hao wamesema, wanataka katiba ya Sweden ipige marufuku kuchezewa mafundisho ya kidini na hasa vitabu vitakatifu vya kidini.

Imam wa msikiti mmoja wa Sweden, Sheikh Husain Farah amesema, hatutaki kuona vitendo viovu vya maadui wa dini vinaonekana ni vya kisheria na hili halihusiani na Qur’ani tu, bali pia vitabu vya Wakristo vya Taurati na Injili.

Jinai inayoendelea hivi sasa huko Sweden ya kuchomwa moto nakala za Qur’ani Tukufu inapingwa na wanasiasa wengi wa nchi hiyo kutoka vyama na mirengo tofauti. Si hayo tu, bali hata Askofu Mkuu wa Swedeni, Antje Jackelén naye amelaani jinai hiyo.

Uchunguzi uliofanywa na taasisi ya utafiti ya PEW unaonesha kuwa, idadi ya Waislamu inazidi kuongezeka katika jamii ya watu milioni 10 ya Sweden, suala ambalo limewatia hamaki maadui wa dini hiyo tukufu ya Mwenyezi Mungu ambao wanafanya njama za kila namna za kuwachokoza Waislamu.

(Visited 47 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!