Tangazo la filamu moja ya vichekesho vya kipuuzi nchini Ufaransa limejeruhi hisia za Waislamu nchini humo na kushinikiza tangazo hilo lifutwe mara moja.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la The Times la Uingereza, matangazo ya filamu ya vichekesho ya BORAT yameenea kila sehemu nchini Ufaransa, kwenye mabasi ya umma, barabarani na kwenye kuta za maeneo tofauti yakimuonesha mcheza filamu mmoja mwanamme anayeshinda wanyama kwa kukosa haya, akiwa amevaa kidani chenye neno takatifu lililoandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Kitendo cha watengeneza filamu hao waliotumia jina takatifu katika sehemu chafu kama hiyo kimewakasirisha mno Waislamu na kushinikiza tangazo hilo liondolewe mara moja.

Hata hivyo watengeneza filamu hiyo (RATP) wamekataa wakidai ni jambo lisilowezekana kabisa.

Pamoja na hayo gazeti la Daily Mail la Uingereza limesema kuwa, baadhi ya mabasi ya umma ya Ufaransa yamelazimika kuondoa tangazo hilo. Mbasi hayo ni yale ya mtandao wa TICE ambayo yanafanya kazi zake katika maeneo yenye Waislamu wengi nchini Ufaransa.

Madereva wengi wa mabasi mjini Paris ambao wengi wao ni Waislamu nao wameelezea kukasirishwa mno na uchokozi huo na kuitaka manispaa ya Paris kuondoa matangazo hayo katika mabasi.

Dereva mmoja anayejulikana kwa jina la Django M. amenukuliwa na gazeti la Daily Mail la Uingereza akitishia kuzichuna picha hizo kama hazitaondolewa.

Tayari Ufaransa imetumbukia kwenye matatizo makubwa kutokana na gazeti la Charlie Hebdo kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na jinai hiyo kuungwa mkono waziwazi na rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron. Malalamiko ya Waislamu na kampeni ya kususia bidhaa za Ufaransa inaendelea katika ulimwengu wa Kiislamu, suala ambalo limemlazimisha rais wa Ufaransa alegeze kamba na kudai amenukuliwa vibaya.

(Visited 28 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!