Maimamu na makhatibu wa misikiti nchini Misri pamoja na  vyuo vya Qur’ani na vituo vya kielimu vya nchi hiyio vimeitaka Wizara ya Wakfu ifungue upya harakati za Qur’ani na elimu baada ya kufungwa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Kwa mujibu wa “Misr al Yaum” maimamu wa sala za jamaa, makhatibu wa misikiti, maqarii, mahufadhi wa Qur’ani, vyuo na maktaba za Qur’ani pamoja na asasi za kielimu za Misri ambazo ziko chini ya Wizara ya Wakfu zimetoa tamko la pamoja na kumtaka Waziri wa Wakfu, Mohamed Mokhtar Gomaa akubali ombi lao la kufunguliwa harakati za Qur’ani na kielimu nchini humo.

Tamko hilo limemtaka Waziri Gomaa afungue vyuo vya Qur’ani na vya kielimu kwa ajili ya kuzidi kueneza fikra sahihi za Kiislamu na kuwalea watoto kwa maadili mazuri na yanayopendeza. Sehemu moja ya tamko hilo imesema: “Tunakuomba ufungue harakati za Qur’ani na za kielimu ili ujumbe wa Uislamu uweze kuwafikia watoto. Tutachunga protokali zote za kiafya. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuondolee ugonjwa na balaa hili (la corona) sisi na walimwengu wote.”

(Visited 19 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!