Wananchi wa Bosnia wamefanya sherehe na tamasha kubwa la kiutamaduni linalojulikana kwa jina la Ayvaz Dede ili kusherehekea mwaka wa 512 wa tangu taifa hilo la Ulaya Mashariki kuingia katika dini tukufu ya Kiislamui.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Anadolu, sherehe hizo zimefanyika kwenye kijiji cha Prusac cha katikati mwa Bosnia Herzegovina kwa maonyesho ya kila namna ya kale.

Ayvaz Dede ni katika sherehe zinazodumu kwa siku nyingi zaidi nchini Bosnia Herzegovina na unahesabiwa kuwa ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa Waislamu barani Ulaya.

Ripoti zinasema kuwa, maelfu ya Wabosnia hujitokeza kila mwaka kuadhimisha mwaka walipoingia katika dini tukufu ya Kiislamu. Sherehe hizo zimechukua jina la mtu ambaye alitoa mchango mkubwa wa kuingia Wabosnia katika dini takatifu ya Kiislamu.

Wakati wa sherehe hizo, wananchi wote wa Bosnia wa rika na wa maeneo tofauti, hukusanyika pamoja katika kijiji hicho cha Prusac cha katikati mwa nchi hiyo, wakiwa wamevaa nguvo za jadi, wengine wakitembea kwa miguu na wengine wakiwa juu ya farasi na vipando vingine.

Sehemu ya sherehe za Wabosnia za kuadhimisha mwaka walipoingia kwenye Uislamu

Mwaka huu sherehe hizo zimefanyika leo Jumamosi, Juni 25, 2022 ambapo wapanda farasi 110 kutoka miji tofauti ya Bosnia wamelekea katika kijiji cha Prusac kwa ajili ya sherehe hizo.

Sherehe hasa zitaanza kesho Jumapili na zitafunguliwa kwa Sala ya Adhuhuri ya jamaa ambayo itasaliwa kwa pamoja na washiriki wa sherehe hizo.

Mapokezi ya kihistoria yanasema kuwa, Ayvaz Dede alikuwa mwenyeji wa eneo la Anatolia la nchini Uturuki ambaye miaka 510 iliyopita, wakati Bosnia ilipokumbwa na ukame mkubwa, alikwenda kwenye kijiji cha Prusac cha katikati mwa Bosnia Herzegovina na kuwaokoa na janga hilo watu wa eneo hilo. Historia inasema kuwa, Ayvaz Dede alifanya ibada za Sala na ibada nyinginezo kwa muda wa siku 40. Baada ya siku 40 alifanikiwa kugundua mto ambao maji yake yalikuwa yanatoka mlimani na kwa njia hiyo aliweza kuwaokoa watu wa eneo hilo na janga hilo. Wabosnia wote waliamua kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu kama shukrani yao kwa Mwenyezi Mungu.

(Visited 34 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!