Mufti wa Quds (Baytul Muqaddas) huko Palestina amesema kuwa, Msikiti wa al Aqsa ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu na una hadhi ya kipekee kwa Waislamu. “Msikiti huo ni mali ya Waislamu hivyo wasio Waislamu hawamiliki chochote katika msikiti huo mtukufu,” amesema.
Gazeti la al Rai al Yaum limemnukuu Mufti wa Quds, Sheikh Muhammad Hussein akisema hayo kwa kusisitiza katika khutba za Sala ya Ijumaa ya jana tarehe 4 Septemba 2020 na kuongeza kuwa, Msikiti wa al Aqsa ni miongoni mwa maeneo matakatifu ya Waislamu na ni mali ya Waislamu tu na suala hilo limetiliwa mkazo pia ndani ya Qur’ani Tukufu.
Amesema, Wakrsito huko Palestina wana makanisa yao na Mayahudi nao wana mahekalu yao hivyo si sahihi kwao kudai chochote katika Msikiti wa al Aqsa.
Amesisitiza kuwa, mtu yeyote atakayefumbia jicho hata shibri ndogo tu ya eneo hilo tukufu la Waislamu ni msaliti mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume Muhammad SAW na mbele ya Waislamu.
Ikumbukwe kuwa Wazayuni wanafanya njama za kukiteka Kibla hicho cha kwanza cha Waislamu kwa madai kuwa ni eneo takatifu kwa Mayahudi. Njama inayofanyika hivi sasa ni kujaribu kugawana eneo na wakati wa kutumia Msikiti huo baina ya Waislamu na Mayahudi.

(Visited 31 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!