Kwa mara ya kwanza, Iran imeipelekea Oman shehena ya tani 2000 za lami. Shehena hiyo imeelekea nchini Oman kutoka kwenye mji wa bandari wa Bandar Lengeh wa kusini mwa Iran.

Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo na kumnukuu Sina Dalai, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha shirika la Petrotar Farasahel akisema kuwa, shehena hiyo imepelekwa nchini Oman kwa kutumia meli moja kubwa.

Ameongeza kuwa, nchi mbili ndugu za Kiislamu za Oman na Iran zitaendelea na biashara hiyo katika siku za usoni. Inatarajiwa kuwa, kila mwezi Iran itakuwa inaipatia Oman tani 20,000 za lami.

Naye Hamed Mohammadi, Naibu wa Mkuu wa Uzalishaji wa Shirika la Petrotar Farasahel huko Bandar Lengeh, kusini mwa Iran amesema kuwa, kwa mwaka shirika hilo linaweza kusafirisha nje lami yenye thamani ya baina ya dola milioni 35 hadi milioni 50.

(Visited 15 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!