Jeshi la polisi limemtia mbaroni mtu mmoja mwenye asili ya Asia baada ya kuenea mkanda wa video katika mitandao yakijamii nchini Kuwait, unaoonesha mtu huyo akikivunjia heshima Kitabu Kitakatifu cha Qur’ani.

Taarifa zimelinukuu jeshi la polisi la Kuwait likithibitisha habari ya kutiwa mbaroni adui huyo wa Uislamu ambaye uhalifu wake huo umewakasirisha mno Waislamu.

Msimamo wa Wizara

Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kuwait imeandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, mtu anayeonekana kwenye mkanda huo wa video ana asili ya Asia na tayari ameshatiwa mbaroni kwa kosa la kuvunjia heshima matukufu ya kidini ya nchi hiyo.

Katika taarifa yake hiyo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kuwait imesema, tayari mtu huyo amekabidhiwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua kali zaidi za kisheria.

Vile vile wizara hiyo imewaomba wananchi kuwa watulivu lakini wakati huo huo imesema, kamwe haiwezi kuvumilia kuona Mwenyezi Mungu na dini yake ya Kiislamu wanavunjiwa heshima na mtu yeyote yule.

(Visited 39 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!