Muhammad Abdul Hadi, baba wa watoto wanne waliozaliwa na upungufu wa kiungo cha macho nchini Saudi Arabia, watatu wanaume na mmoja mwanamke, amepata taufiki ya kuwalea vizuri watoto wake hao na kuwasomesha elimu mbalimbali hususan hifdh ya Qur’ani Tukufu.

Mtandao wa habari wa “Akhbar 24” umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, watoto hao wanne waliozaliwa na upungufu wa kuona, wameweza kushinda upungufu wao huo wa kimwili, kuwa imara na kupata mafanikio katika masuala mengi.

Watoto hao wanne waliohifadhi Qur’ani Tukufu licha ya kwamba wamezaliwa hawaoni, wanawashukuru sana baba na mama kwa juhudi zao kubwa zilizowasaidia kushinda changamoto za upungufu huo walio nao mwilini na kuwaimarisha kiroho na kielimu. Wanasema, sasa hivi wanajivunia kuzaliwa na wazazi hao wawili, wanahisi ni watu muhimu katika jamii na wanajiona hawana upungufu wowote katika miili yao.

Bw. Muhammad al Abd al Hadi, baba wa watoto hao wenye upungufu wa nuru ya macho lakini waliohifadhi Qur’ani anasema: Wanangu wanapeana moyo na wanajiamini. Na mimi najivunia kuwa na watoto wenye moyo kama hawa.

Abdul Hadi ni mtoto wa kiume mkubwa katika familia hiyo ya watu wa Qur’ani. Anasema, pamoja na kuzaliwa kwetu na upungufu huu wa viungo muhimu mwilini, lakini tunaendelea na masomo yetu kama kawaida pamoja na watoto wengine wasio na upungufu kama wetu. Isipokuwa tu katika masomo kama ya hisabati, sayansi, lugha ya Kiingereza na kompyuta tunasomeshwa na wataalamu waliojikita kwenye usomeshaji wa watoto wasioona. Munira ni mtoto wa kike wa familia hiyo. Anasema, upungufu wake wa kuona haukumzuia kuendelea vizuri na masomo na kutafuta elimu zote. Anasema, licha ya kwamba anakumbana na changamoto nyingi, lakini amefanikiwa kupata elimu na maarifa na kuhifadhi Qur’ani Tukufu kutokana na baba na mama yake kumpa nguvu za kujiamini, kumuhamasisha na kumuondolea kabisa fikra kwamba ana upungufu wa kiungo muhimu mwilini mwake.

(Visited 6 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!