Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka serikali za nchi za dunia kutilia maanani jinsi ugonjwa wa COVID-19 ulivyosaidia kuboreka hali ya hewa katika kona zote za dunia (kutokana na kupungua mno safari za vyombo vinavyoharibu mazingira duniani).
António Guterres amesema hayo wakati akizungumza na mawaziri kwa njia ya video kuhusiana na upande wa pili wa matokeo ya ugonjwa wa corona na kusema kuwa sasa hivi dunia inakabiliwa na masuala mawili, kupambana na ugonjwa wa COVID-19 na mabadiliko ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kusaidia kuongezeka kiwango cha mvua katika nchi ya Benin ya magharibi mwa Afrika.
“Wacha tuyashughulikiea masuala yote hayo mawili kwa njia sahihi ili kuviandalia matumaini mazuri vizazi vijavyo, sasa hivi ni wakati muhimu sana kwa walimwengu na kwa sayari ya dunia” amesema Guterres kwa njia ya video.
Mkutano huo wa mawaziri umeitishwa na serikali ya Japan na kushirikisha maafisa wa ngazi za juu wa nchi mbalimbali pamoja na wawakilishi wa makundi ya vijana, asasi za kijamii, mashirika, wafanyabiashara na serikali za kieneo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaja hatua sita chanya zinazopaswa kuchukuliwa kwa ajili ya kuisaidia hali ya hewa duniani kuwa ni pamoja na kuwekeza katika kazi zinazohusiana na mimea na miti, kutovumilia viwanda vinavyochafua hali ya hewa, kukabiliana na matumizi makubwa ya nishati ya fosili n.k.

(Visited 14 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!