Mahakama ya umma nchini Uingereza imetoa taarifa ya kukubali kufuatilia ombi la Kongamano la Kimataifa la Uyghur la kufuatilia uvunjaji wa haki za binadamu na uwezekano wa kuweko mauaji ya umati dhidi ya Waislamu wa jamii hiyo nchini China.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti habari hiyo na kusema kuwa mahakama ya umma ya Uingereza imekubali ombi la wakili mmoja wa haki za binadamu anayewakilisha Kongamano la Kimataifa la Uyghur la kuiomba mahakama hiyo ifuatilie madai ya kuvunjwa haki za Waislamu wa Uyghur wa kabila la Kituruki huko mashariki mwa China.

Kwa mujibu wa Kongamano la Kimataifa la Uyghur, Geoffrey Nice, wakili wa masuala ya haki za binadamu ameitaka mahakama hiyo ifanye uchunguzi kuhusu uwezekano wa kuendelea kuweko jinai na mauaji ya kizazi cha Waislamu wa Uyghur nchini China.

Inatarajiwa kuwa mahakama hiyo itaanza kusikiliza mashtaka hayo mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2021.

Miongoni mwa masuala muhimu yanayotarajiwa kushuhudiwa kwenye vikao vya kusikiliza kesi hiyo ni ushahidi kuhusu kuhusika serikali ya China katika madai ya kuvunja haki za Waislamu wa jamii ya Uyghur mashariki mwa nchi hiyo.

Wakili Nice amesema kamwe madai ya kuweko mauaji ya umati hayatosikilizwa kwenye vikao vya wazi vya mahakama hiyo.

Amesema, madai ya kuweko kambi za kuwafanyisha kazi za lazima Waislamu na kuwakata kizazi ni miongoni mwa ushahidi wa uvunjaji wa makubaliano ya kimataifa ya kukabiliana na mauaji ya umati ambao utatolewa na kusikilizwa kwenye mahakama hiyo.

(Visited 67 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!