Polisi wa Israel wamewazuia Wapalestina 2,000 kuingia katika Kibla cha Kwanza cha Waislamu, yaani Msikiti wa al Aqsa kwa madai ya kutokuwa na vibali.

Mtandao wa Kiarabu wa televisheni ya Russia iitwayo “Rusia al Yaum” umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, jana Ijumaa, polisi wa Israel waliwazuia Waislamu 2,000 wanaoishi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wasiingie katika Masjid al Aqswa kwa kukosa vibali. Mamia ya Waislamu wote hao walishindwa kushiriki katika Sala ya Ijumaa hiyo jana.

Katika taarifa yake, jeshi la polisi la Israel limedai kuwa, tangu asubuhi hadi mchana walikuwa na operesheni ya kuwazuia Wapalestina kuingia katika Msikiti wa al Aqsa na wote walikuwa wanawarejesha Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kwa mabasi. Israel inawawekea vizuizi vingi Wapalestina ili wasiingie katika Msikiti wa al Aqsa hasa wale wanaoishi Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

(Visited 3 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!