Baraza la Sanate la jimbo la Michigan limepasisha na kutambua rasmi maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hijab ambayo ni tarehe Mosi Februari.

Tovuti ya Odisha imeinukuu redio WDET 101.9FM ikitangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, sambamba na nchi 150 kuadhimisha Siku ya Hijab Duniani ambayo ni tarehe Mosi Februari, Baraza la Sanate la jimbo la Michigan, nalo limepasisha na kutambua rasmi maadhimisho ya siku hiyo kwenye jimbo hilo. 

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, sasa hivi kuna Waislamu 300,000 wanaishi katika jimbo hilo la magharibi mwa Marekani.

Seneta Bi Stephanie Chang ndiye aliyependekeza muswada huo kwa Baraza la Sanate la Michigan na hatimaye umepasishwa.

Bi Chang amesema, Siku ya Kimataifa ya Hijab ni siku ya mshikamano na ni siku ya kutambua uwepo wa mamilioni ya Waislamu duniani na wajibu kwa wanadamu wote kuishi pamoja kwa usalama na amani. Huu ni mwito wa wazi kwa kila mwanamke popote alipo na wa tabaka lolote kwamba kuna haja kwetu sote kutangaza mshikamano wetu na wanawake wenzetu wa dini ya Kiislamu na tuwe pamoja nao. 

Bi Nazma Khan, Mwasisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Siku ya Kimataifa ya Hijab amesema, taasisi yake hiyo si ya kiserikali na si ya kibiashara, bali ni kwa ajili ya kutoa elimu kwa watu kuhusu vazi la staha ya mwanake wa Kiislamu yaani Hijab.

(Visited 46 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!